tgindex
KIDIGITALI | LEARN with ALLY

KIDIGITALI | LEARN with ALLY

Статистика

Learn everything about Online Hustling, One Person Business, Productivity, Monetization and Growth. My page is about mindset shift, if you’re open to learning new things, let’s connect. For Business: DM @allymsangi Email: ally@allymsangi.com

Последний пост
16 авг.
Последнее чтение
01:56
Постов за неделю
11
Всего постов
29
Тип
открытый
Язык
английский
Категория
Новости и СМИ (по похожим)
В каталоге с
13 авг.
Подписчики
1 110
−11 за 5 дн.
Сутки
−2
−0,18%
Неделя
 
Месяц
 
Просмотров на пост
41
29 постов
Вовлечённость
3,7%
к подписчикам
Постов в день
1,6
всего 29
Упоминаний
0
каналов
Охват размещения
оценка
1/24сутки в ленте
30
1/48двое суток
34
1/72трое суток
37

Оценка по просмотрам недавних постов: пост набирает почти всё за первые сутки.

Посты

  • Unapofanya Mabadiliko kwenye Career yako, basi fanya kama TARZAN. Kuna watu wana tamani kubadilisha career zao, kuacha kazi zao za sasa na kuanza kitu kipya wanachokipenda zaidi. Lakini kuna shida moja... wengi wanadhani ili waanze maisha mapya, lazima kwanza waache kabisa yale ya zamani. Sasa hapa ndipo wengi wanafanya MISTAKE. Ebu fikiria Tarzan yule wa kwenye movie ile ya wanyama anavyohama kutoka mti mmoja kwenda mwingine. Hajiangushi kutoka kwenye tawi la kwanza akiwa na matumaini kwamba atafika kwenye tawi linalofuata. Anachofanya ni anashika tawi jipya kwanza, ndipo anaachia la zamani. Sasa hii ni principle nzuri sana kwenye career na biashara na hata kwenye maisha kwa ujumla tu. Unataka kuacha ajira yako na kuanza biashara? Usikimbilie kuacha kwanza. Anza biashara pembeni. Jifunze. Pata wateja wako wa kwanza. Anza kupata income. Jenga confidence. Halafu biashara yako ikianza kuwa na uwezo wa kukushikilia, ndipo uanze kufikiria kuachia ajira. Unataka kuingia kwenye freelancing? Usisubiri mpaka uwe unemployed. Anza kupata clients ukiwa bado una kazi yako. Unataka kuwa creator? Anza kutengeneza content kabla hujaacha kazi. Unataka kuhamia kwenye biashara? I-test kwanza kabla hujaweka maisha yako yote kwenye hiyo idea. Usiache chanzo chako cha income kabla hujajenga kinachofuata. Sio woga. Ni STRATEGY. Kwa sababu mabadiliko mazuri hayahitaji uruke kutoka kwenye maisha yako ya sasa kwenda kwenye usiyo yajua. Tengeneza daraja wakati bado umesimama upande huu. Halafu vuka ukiwa tayari. Ninapo sema badili Career yako kama TARZAN... Nina maanisha usichie TAWI la zamani kabla haujashika jipya. Nadhani umenielewa vyema. PS: Kama unataka kujifunza jinsi ya kutumia internet kujenga income yako mwenyewe, soma THE INTERNET ATM 📖 ni TSh 23,000 tu. Kupata copy yako, nicheki WhatsApp 0712988589.

  • USITUMIE KILA PESA UNAYOIPATA. JENGA KITU KITAKACHOKULETEA PESA TENA. Watu wengi wanapoongeza kipato, huanza kuongeza matumizi pia. Anapata mshahara mkubwa zaidi, anabadilisha simu, anaongeza gharama za maisha na baada ya muda anarudi kusema kuwa pesa bado haitoshi. Robert Kiyosaki katika kitabu chake Rich Dad Poor Dad alisisitiza umuhimu wa kujenga assets badala ya kutegemea kipato pekee. Maana yake ni kwamba, usifikirie tu namna ya kupata pesa nyingi zaidi, fikiria pia namna ya kutumia pesa uliyonayo kujenga kitu kitakachoweza kukuletea value tena. Kwa mfano, unaweza kutumia Tsh 500,000 kununua kitu ambacho kitakupa furaha kwa muda mfupi, au ukatumia sehemu yake kujifunza skill, kutengeneza digital product, kuanzisha website, kujenga audience au kuwekeza kwenye biashara ndogo. Vyote vinahitaji pesa, lakini havina matokeo sawa. Tatizo sio kutumia pesa. Tatizo ni kutumia kila pesa bila kujenga chochote kinachoweza kukusaidia kesho. Hata smartphone uliyonayo inaweza kuwa asset kama inakusaidia kujenga audience, kutengeneza content, kuuza huduma, kujenga biashara au kutengeneza digital products. Lakini kama inatumika zaidi kuangalia watu wengine wakijenga maisha yao, bado ni kifaa tu. Siku unapopata pesa, usijiulize tu, “Nitanunua nini?” Jiulize pia, “Nitaijenga nini kwa pesa hii?” Kwa sababu kuna tofauti kubwa kati ya mtu anayefanya kazi ili kupata pesa na mtu anayefanya kazi huku akitumia sehemu ya kipato chake kujenga assets. Mmoja anaanza kila mwezi kutoka zero. Mwingine anajenga kitu kidogo kidogo ambacho kinaweza kuendelea kumsaidia hata kesho. Usitumie kipato chako kuongeza tu kiwango cha maisha yako. Tumia sehemu yake kuongeza uwezo wako wa kutengeneza kipato zaidi. Hapo ndipo pesa inaanza kukufanyia kazi badala ya wewe kuanza upya kila mwezi.

  • 8. Kuelewa namna ya kujenga income kupitia skills zako, hata kama huna office, kampuni kubwa au mtaji mkubwa. 9. Kujua namna ya kuanza kutoka ZERO bila kusubiri uwe na kila kitu kwanza. 10. Kuelewa kwa nini kuwa na Internet pekee hakutoshi. Unahitaji kujua unauza nini, unamuuzia nani na kwa nini akulipe. 11. Kujifunza namna ya kugeuza skill moja kuwa huduma, huduma kuwa clients, na clients kuwa income. 12. Kugundua opportunities ambazo tayari zipo kwenye Internet lakini watu wengi hawazioni kwa sababu wanatafuta “AJIRA” badala ya kutafuta MATATIZO YA KUTATUA. 13. Kujenga mindset ya mtu anayejua kutumia Internet kama economic tool, si sehemu ya ku-scroll TikTok, Instagram na YouTube tu. 14. Kuelewa namna ya kuanza kujenga income stream ambayo inaweza kukua pamoja na skill, reputation na audience yako. 15. Na muhimu zaidi, kutoka kwenye swali la: “NITAPATA WAPI KAZI?” kwenda kwenye: “NI TATIZO GANI NAWEZA KULITATUA KWA KUTUMIA INTERNET?” Kwa kifupi: THE INTERNET ATM inakufundisha kuiona Internet kama platform ya kujenga income, si sehemu ya kutumia muda tu. Huhitaji kuwa programmer. Huhitaji kuwa influencer. Huhitaji kuanza na ofisi. Huhitaji kusubiri uwe expert wa kila kitu. Unahitaji kujua unacho uwezo wa kufanya, soko linahitaji nini, na namna ya kuunganisha vitu hivyo viwili. Kama wewe ni kijana unayetafuta namna ya kuanza kutengeneza kipato online, freelancer, content creator, student, entrepreneur au mtu ambaye amekuwa akisema: “Nataka kuanza online lakini sijui nianzie wapi.” Hiki kitabu kimeandikwa kwa ajili yako. THE INTERNET ATM Turn your skills, the Internet and opportunities into income. 📖 Kupata kitabu: Nicheki WhatsApp 0712988589

  • THE INTERNET ATM si kitabu cha kukufundisha “jinsi ya kupata hela online” kwa story za motivation. Ni kitabu cha kubadilisha namna unavyofikiria kuhusu SKILLS, INTERNET, OPPORTUNITIES na INCOME. Ukipata The Internet ATM, utaweza: 1. Kuelewa namna Internet ilivyobadilisha njia ambazo mtu anaweza kutengeneza kipato bila kuanza na mtaji mkubwa. 2. Kujua business models ambazo unaweza kuanza kwa kutumia skill, simu/laptop na Internet. 3. Kujua ni skills zipi zinaweza kugeuzwa kuwa huduma ambazo watu na biashara wako tayari kulipia. 4. Kujifunza namna ya kuangalia tatizo la mtu kama opportunity ya kutengeneza pesa. 5. Kuelewa tofauti kati ya kujifunza skill na kujua namna ya kuifanya skill hiyo ikuletee income. 6. Kujua namna ya kutumia AI kama ChatGPT kuongeza uwezo wako na kufanya kazi ambazo zamani zilihitaji muda na resources nyingi. 7. Kujifunza namna ya kutumia CONTENT kama asset, badala ya kupost kila siku bila kujua inakusaidiaje kutengeneza pesa.

  • Kuna mtu amenifuata kwenye DM, akaniambia... “Kaka Ali, TSh 23,000 ni nyingi sana kwa kitabu.” Hebu fikiria TSh 23,000 kama pesa, si kama bei ya KITABU. Pesa hii inaweza kuishia kwenye matumizi madogo ya kawaida, ukaamka kesho na hakuna kitu cha maana kinachobaki. Au unaweza kuiweka kwenye kitu ambacho kinaweza kubadilisha namna unavyoitumia Internet. THE INTERNET ATM imeandikwa kwa mtu anayetaka kuanza kutengeneza kipato online lakini hajui aanzie wapi. Ndani yake utaona business models, skills zinazoweza kuuzwa, opportunities za Internet, matumizi ya AI na namna ya kugeuza uwezo wako kuwa income. Si MOTIVATION ya siku mbili. Ni ramani ya kuanzia. Na ukipata hata mteja mmoja kutokana na kitu ulichojifunza ndani yake, TSh 23,000 inaweza kuwa moja ya pesa ndogo zaidi ulizowahi kuwekeza kwenye uwezo wako. THE INTERNET ATM 📖 ni TSh 23,000 tu. Kupata copy yako, nicheki WhatsApp: 0712988589

  • Kama Bado haujapata kitabu cha THE INTERNET ATM Nitafute WhatsApp 0712988589 Andika “THE INTERNET ATM”

  • Your biggest asset isn't your followers. It's the community that trusts you. Anyone can gain views. Anyone can go viral. But very few people build an audience that listens, engages, and comes back every time they post. If you want to build a business with content, stop chasing numbers and start building relationships. Show up consistently. Give people a reason to follow you. Share your wins. Share your failures. Take them behind the scenes. Answer their questions. Ask for their opinions. Let them be part of your journey. People don't just buy products. They buy trust. And trust is built one valuable post at a time.

  • Kuna watu wanatumia internet kutumia pesa. Wengine wanaitumia kutengeneza pesa. Wewe uko upande gani? Kama unataka kuhamia upande wa wanaotengeneza pesa, kitabu changu cha THE INTERNET ATM kinakufundisha mfumo huo kwa Kiswahili, hatua kwa hatua. Bei yake ni Tsh 23,000 tu. 📲 Nicheki WhatsApp 0712988589 andika "THE INTERNET ATM"

  • YouTube imebadilisha masharti ya monetization, na kama una mpango wa kuanza kupata pesa kupitia YouTube, hili ni jambo la kuanza kulifuatilia sasa. Kuanzia February 1, 2027, YouTube itaongeza kiwango cha mahitaji kwa creators wapya wanaotaka kuingia kwenye YouTube Partner Program (YPP) na kupata mapato ya matangazo. Kwa sasa unahitaji subscribers 1,000 pamoja na mojawapo ya haya: • Watch hours 4,000 ndani ya miezi 12 • Au views milioni 10 za Shorts ndani ya siku 90. Lakini kuanzia Februari 2027, mahitaji hayo yatakuwa: • Subscribers 1,000 • Watch hours 8,000 ndani ya siku 365 AU • Views milioni 20 za Shorts ndani ya siku 90. Kwa kifupi, YouTube imeongeza mara mbili kiwango cha watch hours na Shorts views kinachohitajika kwa creators wapya kupata mapato ya matangazo. Lakini kuna jambo muhimu sana. Kama tayari uko kwenye YouTube Partner Program, mabadiliko haya ya entry requirements hayakutoi kwenye YPP. YouTube imesema hayataathiri creators ambao tayari wako kwenye programu. Pia, kiwango cha chini cha kupata access ya baadhi ya features kama Fan Funding na Shopping hakijabadilika. Bado unaweza kufikia hatua hiyo ukiwa na subscribers 500 pamoja na watch hours 3,000 ndani ya miezi 12, au Shorts views milioni 3 ndani ya siku 90. Kuna pia mabadiliko muhimu kwa Shorts. Kwa creators ambao tayari wako YPP, YouTube itaweka kiwango cha views milioni 10 za Shorts ndani ya siku 90 kwa ajili ya kuendelea kupata mapato kutoka kwenye Shorts ad revenue sharing. Ukianguka chini ya kiwango hicho, mapato ya Shorts yanaweza kusimama mpaka ufikie tena threshold hiyo. Hii ni tofauti na monetization ya long-form videos. Lakini usipaniki.  Mabadiliko haya hayajaanza bado. Una mpaka February 1, 2027 kabla ya requirements mpya kuanza kutumika. Hiyo inamaanisha bado una nafasi ya kufikia requirements za sasa ambazo ni watch hours 4,000 au Shorts views milioni 10. Kwa hiyo kama ulikuwa unasema... “Nitaanza YouTube mwaka ujao.” Labda ni muda wa kuanza sasa. Anza kujenga channel. Anza kutengeneza videos. Anza kukusanya subscribers. Anza kukusanya watch hours. Kwa sababu kuanzia Februari 2027, safari ya kufikia ad monetization kwa creators wapya itakuwa ngumu zaidi (Sio kama haiwezekani). Je! Utaanza kabla kiwango hakijapanda?

  • Biashara Hii Inaweza Kukulipa Tsh 100,000 hadi 500,000 kwa Bidhaa Moja Tu Leo ngoja nikupe idea ambayo watu wengi wanaipuuzia, lakini inaweza kukuletea kipato kikubwa. Biashara ya kuuza vitu USED. Na jambo zuri zaidi ni kwamba, unaweza kuanza hata kama huna mtaji. Kinachohitajika si pesa nyingi. Kinachohitajika ni uwezo wa kuona fursa, kufanya negotiation, na kujua kuuza. Mfano, mtu anataka kuuza Laptop yake. Akisema anahitaji Tsh 500,000, wewe kubaliana naye hiyo ndiyo pesa yake ya mwisho. Piga picha nzuri, andika maelezo yanayovutia, kisha itangaze kwa Tsh 700,000. Ukipata mnunuzi, mmiliki anachukua Tsh 500,000. Wewe unabaki na Tsh 200,000 kama faida. Hujanunua Laptop. Hujatumia mtaji. Lakini umetengeneza pesa. Ukifanya hivyo mara kwa mara, utaanza kukusanya mtaji wako mwenyewe. Baadaye hutasubiri tena kuwa dalali. Utakuwa unanunua bidhaa moja kwa moja na kuuza kwa faida kubwa zaidi. Na hii siyo kwenye Laptop pekee (Hii nimekupa kama mfano tu). TV, Fridge, sofa, simu, AC, mashine za kufulia, furniture, hata magari. Mfumo ni uleule tu. Unanunua kwa bei nzuri au unapata makubaliano mazuri, halafu unauza kwa thamani ya soko. Ndio maana kuna watu wanaingiza Tsh 100,000 hadi 500,000 kwa kuuza bidhaa moja tu. Ukiona watu wanaouza magari wakikupa bei ya chini, si kwa sababu gari lako halina thamani. Mara nyingi wanahakikisha wanabaki na nafasi ya kupata faida watakapo liuza. Huo ndiyo mfumo wa biashara. Tatizo ni letu wa bongo ni moja tu, wengi wamefundishwa kutafuta mtaji kabla ya kutafuta fursa. Wafanyabiashara wanao fanikiwa wanaanza kwa kutafuta fursa, halafu mtaji unafuata baadae. Usikubali kukosa kipato kwa sababu tu huna mtaji. Mara nyingi unacho kikosa si pesa. Ni mfumo wa kuziona na kuzitumia fursa.

  • PESA yoyote ile unayo itaka tayari ipo. Tatizo ni kwamba haipo kwenye mfuko wako. Ipo kwenye mfuko wa mtu mwingine. Kuna mtu anataka website. Mwingine anataka logo. Mwingine anataka content. Mwingine anataka kuuza bidhaa zake. Na mwingine anataka kujifunza skill. Mwingine anataka kupata wateja. Alafu kuna mwingine anataka mtu amsimamie social media zake. PESA IPO. Unacho takiwa ni kujiuliza swali hili tu... Je, una njia ya kuifikia? Hapa ndipo watu wengi wanaelewa vibaya kuhusu internet. Wanafikiri ili utengeneze pesa online lazima uwe na bidhaa. SIO LAZIMA. Wengine wanafikiri lazima uwe na mtaji. Sio lazima. Wengine wanafikiri lazima uwe influencer. Sio lazima. Unachohitaji kwanza ni vitu vitatu... SKILL + ATTENTION + TRUST. Uwe na kitu unachoweza kufanya. Watu wajue kwamba unaweza kukifanya. Na wakuamini kiasi cha kukulipa. Hapo ndipo THE INTERNET ATM inaanza kufanya kazi Sasa. Ebu fikiria ATM ya kawaida tu. ATM yenyewe haina pesa yako. Inakupa access kwenye pesa iliyo kwenye account yako. Internet nayo ni hivyo hivyo. Internet haikutengenezei pesa kwa uchawi. Inakupa access kwa mamilioni ya watu ambao tayari wana pesa, wana matatizo, wana mahitaji, na wako tayari kulipa mtu anaye weza kuyatatua. Ndio maana mtu mwenye laptop na skill moja anaweza kuanza kupata pesa bila kuwa na office. Anaweza kuandika. Anaweza design. Anaweza edit video. Anaweza kutengeneza websites. Anaweza kuuza. Anaweza kufundisha. Anaweza kusimamia accounts za watu. Anaweza kutengeneza digital products. Anaweza hata kuuza bidhaa za mtu mwingine na kuchukua commission. Hatengenezi pesa kutoka hewani tu. Anahamisha pesa kutoka kwenye mfuko wa mtu mwingine kwenda kwenye mfuko wake kwa kutoa value. Na hapa ndipo kuna SIRI ambayo watu wengi hawajaiona... Huhitaji kuwa na watu wengi. Unahitaji kuwa na access kwa watu SAHIHI. Follower 100,000 ambao hawahitaji unachouza wanaweza kuwa na thamani ndogo kuliko watu 500 wanao kuhitaji. Ndiyo maana nimeipa eBook yangu jina la "THE INTERNET ATM". Sio kwa sababu internet ni mashine ya kutoa pesa. Bali kwa sababu ukiielewa vizuri, internet inakuwa njia yako ya kufikia watu... Huu ni mfumo. PEOPLE → PROBLEMS → VALUE → MONEY. Na ukishajua kutumia mfumo huo, unaanza kuacha kuuliza... "Nitawezaje kupata pesa?" Unaanza kuuliza... "Ni nani ana tatizo ambalo ninaweza kulitatua?" Hapo ndipo utaona mambo kwa jicho tofauti. Kwa sababu pesa nyingi hazipatikani kwa kuitafuta. Zinapatikana kwa kutatua matatizo ya watu ambao wana uwezo wa kulipa. Hiyo ndiyo theory ya THE INTERNET ATM. PS: Kama Bado haujapata kitabu cha THE INTERNET ATM nitafute WhatsApp 0712988589 Andika “THE INTERNET ATM”. Bei yake ni Tsh 23,000 Tu.

  • Kama tayari unatafuta njia ya kutengeneza pesa mtandaoni au bado hujaanza kabisa, hakikisha unajifunza mfumo ambao unaweza kukuletea kipato bila kutegemea bahati. Hizi si nadharia za mtandaoni. Ni mfumo ambao nimetumia kwa miaka mingi kujenga biashara za mtandaoni, kukuza audience, na kutengeneza kipato kupitia internet. Nimekusanya kila kitu kwenye kitabu changu cha THE INTERNET ATM, na nimeelezea hatua kwa hatua kwa Lugha ya Kiswahili ili mtu yeyote aweze kuelewa na kuanza kutekeleza. Kama unataka kujifunza jinsi ya kutumia internet kama chanzo cha mapato, hiki ndicho kitabu cha kuanzia. Tuma ujumbe WhatsApp 0712988589 andika "THE INTERNET ATM"

  • Join My WhatsApp Channel👇 https://allymsangi.com/Whatsappchannel

  • Mabadiliko makubwa kwa wanaolipwa na X (Twitter) Leo, tarehe 8 Agosti 2026 , X imetangaza rasmi kusitisha mpango wake wa malipo wa Creator Revenue Sharing. Kwa waliopo kwenye program hiyo kwa sasa: • Mtaendelea kulipwa mapato mliyoyapata hadi 7 Septemba 2026. • Kutakuwa na malipo ya kawaida tarehe 14 Agosti na 28 Agosti. • Baada ya hapo kutakuwa na malipo ya mwisho tarehe 11 Septemba 2026 kwa mapato yote yaliyopatikana hadi 7 Septemba. Baada ya hapo, program hiyo itafungwa rasmi. X imeleta nini badala yake? Kuanzia 8 Septemba 2026, X inaanzisha program mpya inayoitwa Original Content Rewards. Tofauti kubwa ni kwamba sasa X inataka kulipa zaidi watu wanaotengeneza Original Content, badala ya wale wanao post au kurudia content za watu wengine. Kwa kifupi, kama content zako zinaonyesha mawazo yako, uzoefu wako, uchambuzi wako, video zako, picha zako au maoni yako ya kipekee, una nafasi kubwa zaidi ya kulipwa. Lakini kama kazi yako ni ku-copy, ku-repost, ku-download na kupakia upya content za wengine, au kufanya edits ndogo kwenye kazi za watu wengine, content hizo hazitastahili kulipwa. Vigezo vya kujiunga na Original Content Rewards • Uwe na miaka 18 au zaidi. • Uishi kwenye nchi ambayo program hii inapatikana. • Account yako isiwe na historia ya kukiuka sheria za X au Monetization. • Uwe na Personal Account au Business Account. • Uwe na angalau Verified Followers 500. • Uwe umefikisha angalau 500,000 Home Timeline Impressions ndani ya siku 90 zilizopita kutoka kwa watumiaji wenye X Premium (Blue Tick). Unatakiwa kufahamu kuwa Impression za kwenye comments au replies hazihesabiwi. Uwe na usajili wa X Premium, Premium+, au Premium Business. Uwe unachapisha Original Content mara kwa mara. Habari njema ni kwamba program ya zamani ilihitaji hadi milioni 5 za impressions, lakini sasa kiwango kimeshushwa hadi 500,000. Hata hivyo, X itaangalia pia ubora na uhalisia wa content zako kabla ya kukubali maombi yako. Je, unaona mabadiliko haya yatawasaidia creators wa Tanzania na Afrika, au yata wafanya wengi washindwe kuingia kwenye monetization? Tuambie maoni yako. 👇

  • Imebaki miezi michache tu kumaliza mwaka. Kwa kumtegemea Mungu, tuendelee kukomaa... Bado tuna muda wa kubadilisha mambo mengi. Tusiache kupiga kazi usiku na mchana. Tusimalize mwaka tukiwa watu wale wale. Tufanye kazi kwa bidii, tuwe na nidhamu na tusikubali udhaifu utushinde. NO WEAKNESS. P.S: Join My WhatsApp Channel👇 https://shorturl.at/IofZX

  • Siku hizi karibu kila mtu anataka kuwa Content Creator. Au Influencer. (Tafadhali never ever call me an influencer 😎) Naelewa kwa nini. Kwa sababu, attention inavutia. Likes, comments, shares na followers vinatupa hisia kwamba tunafanya kitu kikubwa. Lakini kuna kitu wengi hawakioni. Wanataka kuwa upande wa kupokea attention. Hawaelewi maisha yaliyopo nyuma ya attention hiyo. Hawaoni pressure ya kutengeneza content kila mara. Hawaoni siku ambazo post zako hazifanyi vizuri. Hawaoni muda unaotumia kujifunza, kuboresha, na kujenga uaminifu wa audience yako. Content Creation si kazi ya kutafuta likes. Ni kazi ya kutengeneza uhusiano na watu. Ukianza kwa kufukuzia attention, utaishia kuchoka. Lakini ukianza kwa kushare unachojua, kutatua matatizo ya watu, na kutengeneza thamani, attention itakuja yenyewe. Ndio maana huwa nawashauri watu waanze kutengeneza content. Sio kwa sababu ni rahisi. Bali kwa sababu ukiifanya kwa sababu sahihi, inaweza kubadilisha maisha yako. Lakini usiingie kwa ajili ya umaarufu. Ingia kwa ajili ya kutoa thamani. Umaarufu unaweza kuja. Trust ndiyo inayobaki.

  • Maarifa yanaweza kubadilisha mwelekeo wa maisha yako, kama utayatumia. Kwa miaka kadhaa iliyopita nimekuwa nikiandika vitabu na kuandaa masterclass kuhusu biashara za mtandaoni, AI, YouTube Automation, Blogging, Freelancing, Affiliate Marketing na Digital Products. Nimeviweka sehemu moja ili iwe rahisi kuvipata kulingana na hatua uliyonayo sasa. Kwa mfano: Unataka kuanza biashara mtandaoni? → The Internet ATM Unataka kujenga Faceless YouTube Channel? → YouTube Automation Masterclass Unatafuta njia za Freelancing? → 100+ Freelance Ideas na How to Start Freelancing Unataka kujifunza Affiliate Marketing? → Affiliate Marketing for Beginners Unataka kutengeneza na kuuza Digital Products? → Digital Product Business Kama kuna maarifa unahisi yana kosekana kwenye safari yako ya kutengeneza biashara mtandaoni, kuna uwezekano utayapata hapa. 🔗 Angalia vitabu na masterclass zote hapa: https://duka.habaritechnology.com/ally-msangi Jifunze. Tekeleza. Jenga Assets. Matokeo yatafuata.

  • Kwa sababu siku moja ya mapumziko haiharibu maendeleo yako. Kinachoharibu maendeleo ni kuacha kabisa. Kwa hiyo... Labda wewe si mvivu. Labda umekuwa ukijaribu kuruka kutoka sifuri hadi mia moja kwa hatua moja. Na maisha hayafanyi kazi hivyo. Mwalimu wa yule kijana wa Martia arts (Samurai) alikuwa sahihi kabisa. Mtu anayeshinda si yule anayejituma sana kwa wiki moja. Ni yule anayejitokeza kila siku. Hata kama maendeleo hayaonekani. Hata kama hatua ni ndogo. Hata kama ni asilimia 1 tu. Miaka mitano ijayo itafika, uwe umefanya chochote au hujafanya. Swali ni moja tu... Je, utaitumia miaka hiyo kusubiri siku ambayo utakuwa tayari... Au utaanza leo, kwa hatua ndogo ambayo utaweza kuirudia kila siku? Kwa sababu mafanikio makubwa... Hayajengwi kwa hatua kubwa. Yanajengwa kwa hatua ndogo zinazorudiwa kila siku.

  • Watu wengi wanafikiri wao ni wavivu. Lakini ukweli ni kwamba... Siyo wavivu. Wamelemewa. Kuna hadithi moja ya zamani kutoka JAPAN. Kijana mmoja aliyekuwa anajifunza martial arts (Kun'gfu) alimfuata mwalimu wake akamuuliza, "Nataka kuwa mpiganaji bora kuliko wote. Itanichukua miaka mingapi?" Mwalimu akamjibu... "Miaka 10." Yule kijana hakuridhika. Akauliza tena, "Na kama nikijituma mara mbili zaidi? Nikafanya mazoezi mchana na usiku bila kupumzika?" Mwalimu akamjibu... "Basi itachukua miaka 20." Jibu hilo linaonekana halina maana. Lakini ukilitafakari vizuri, linafundisha kitu kikubwa sana kuhusu mafanikio. Tatizo la watu wengi si kwamba hawana ndoto. Tatizo ni kwamba wana ndoto nyingi kwa wakati mmoja. Unataka kupunguza uzito. Unataka kuanzisha biashara. Unataka kujifunza AI. Unataka kutengeneza pesa mtandaoni. Unataka kusoma vitabu. Unataka kuamka saa 11 alfajiri. Unataka kuacha kutumia simu kupita kiasi. Unataka kila kitu kibadilike... leo leo tu. Mwisho wake unajikuta hujaanza hata kimoja. Halafu una jiambia... "Mimi ni mvivu." Lakini hebu fikiria. Je, mtu mvivu huwa anajisikia vibaya kwa kupoteza muda? HAPANA. Mvivu huwa hana hata shida. Lakini wewe kila usiku unajilaumu. Unaona kabisa ungeweza kufanya zaidi. Hiyo si dalili ya uvivu. Ni dalili kwamba una ndoto kubwa... Lakini umebeba nyingi kuliko ubongo wako unavyoweza kushughulikia kwa wakati mmoja. Na ubongo ukilemewa... Hutafuta sehemu rahisi ya kukimbilia. Ndiyo maana badala ya kuanza kazi... Unaanza kufungua TikTok. Instagram. Facebook. Au YouTube. Siyo kwa sababu hupendi mafanikio. Ni kwa sababu ubongo unatafuta mapumziko kutokana na presha ya maamuzi mengi. Ndiyo maana motisha peke yake haitoshi. Tatizo si motisha. Tatizo ni kwamba unajaribu kubadilisha maisha yako yote kwa siku moja. Hapo ndipo watu wengi huanguka. Jumapili usiku unaandika ratiba mpya. Kesho utaenda gym. Utasoma kurasa 30. Utafanya biashara saa mbili. Utalala mapema. Hautaingia kwenye mitandao ya kijamii. Utakunywa maji mengi. Ifikapo Jumanne... Ratiba yote imekufa. Halafu unaamini huna nidhamu. Si kweli. Umeanza na mzigo mkubwa kuliko uwezo wako wa kuubeba. Wajapani waligundua suluhisho hili miaka mingi iliyopita. Wakaliita KAIZEN. Maana yake ni... Kuboresha maisha yako kidogo kidogo, kila siku. Si mabadiliko makubwa. Si miujiza. Ni hatua ndogo zinazojirudia kila siku. Ebu ngoja nikwambie hii siri. Ukiboresha maisha yako kwa asilimia 1 tu kila siku... Baada ya mwaka mmoja utakuwa mbali sana na ulipoanza. Tatizo ni kwamba asilimia 1 inaonekana ndogo. Ubongo unapenda matokeo makubwa. Lakini mafanikio makubwa hutokana na hatua ndogo zinazorudiwa kila siku. Sasa ufanye nini? Kwanza... Usijaribu kurekebisha kila kitu. Chagua kitu kimoja tu. Kama ni afya. Basi afya pekee. Kama ni biashara. Basi biashara pekee. Usianze vitu kumi kwa siku moja. Pili... Punguza lengo lako mpaka lisiwe na sababu ya kushindwa. Usiseme utafanya mazoezi saa moja. Sema tu utavaa viatu vya mazoezi. Usiseme utasoma sura nzima. Sema utafungua kitabu. Usiseme utaandika kurasa tano. Sema utaandika sentensi moja. Inaonekana ni ndogo sana. Lakini hapo ndipo siri ilipo. Kwa sababu sehemu ngumu si kufanya. Sehemu ngumu ni kuanza. Ukishavaa viatu... Mara nyingi utaendelea kutembea. Ukishafungua kitabu... Mara nyingi utasoma hata ukurasa mmoja. Hatua ndogo ndiyo inayovunja ukuta wa uvivu. Tatu... Unganisha tabia mpya na kitu ambacho tayari unafanya kila siku. Baada ya kunywa chai. Baada ya kupiga mswaki. Baada ya kula. Usiongeze muda mpya. Tumia muda ambao tayari upo. Halafu... Fuatilia maendeleo yako. Weka alama ya ✔️ kwenye kalenda kila siku unapotekeleza lengo lako. Baada ya siku chache utaona mfululizo wa alama. Na hutataka kuuvunja. Lakini kuna jambo muhimu zaidi. Siku moja utashindwa. Utachoka. Utakuwa bize. Utasahau. Hilo ni la kawaida. Sheria ni moja tu. Usikose siku mbili mfululizo. Ukikosa leo... Rudi kesho. Usisubiri Jumatatu. Usisubiri mwezi mpya. Usijilaumu. Rudi tu.

  • 2010, watu walitengeneza utajiri kupitia Blogs. 2015, YouTube ikabadilisha maisha ya watu wengi. 2020, eCommerce ikatoa mabilionea wapya. 2026/2027? Nina amini ni zamu ya Digital Assets. Ebook. Course. Template. AI Prompt. Newsletter. Membership. Community. Hizi ni bidhaa unazo tengeneza mara moja, lakini unaweza kuziuza tena na tena. Na jambo zuri zaidi? Huhitaji ofisi kubwa. Huhitaji mtaji mkubwa. Unachohitaji ni idea moja nzuri, Google Docs, ChatGPT au Claude, na saa moja kila siku. Miaka michache ijayo, tofauti haitakuwa nani anafanya kazi kwa bidii zaidi. Itakuwa nani anatengeneza assets zinazo muingizia kipato hata akiwa amelala.