- Последний пост
- 15 авг.
- Последнее чтение
- 15 авг.
- Постов за неделю
- 187
- Всего постов
- 376
- Тип
- открытый
- Язык
- sn
- Категория
- Новости и СМИ
- В каталоге с
- 12 авг.
- 1/24сутки в ленте
- 5
- 1/48двое суток
- 5
- 1/72трое суток
- 6
Оценка по просмотрам недавних постов: пост набирает почти всё за первые сутки.
Посты
️️➟ @HabariTz ✰✰✰ DW Kiswahili #duniayetuleomchana: Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) limehimiza umuhimu wa kukiri ukweli kwanza kwa kile kilichotokea nchini humo wakati na baada ya uchaguzi wa Oktoba 29, likisema hatua hiyo ni muhimu kabla ya kuingia katika hatua nyingine za kuliponya taifa. Hayo ni kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa TEC, Padri Charles Kitima, alipozungumza na DW. Padri Kitima ameeleza yaliyojadiliwa kati ya maaskofu hao na Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan katika mkutano wao uliofanyika Agosti 10 mjini Chamwino, Dodoma.
️️➟ @HabariTz ✰✰✰ DW Kiswahili Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) limehimiza umuhimu wa kukiri ukweli kwanza kwa kile kilichotokea nchini humo wakati na baada ya uchaguzi wa Oktoba 29. Limesema hatua hiyo ni muhimu kabla ya kuingia katika hatua nyingine za kuliponya taifa. Hayo ni kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa TEC, Padri Charles Kitima, alipozungumza na DW. Padri Kitima pia alieleza yaliyojadiliwa kati ya maaskofu hao na Rais Samia Suluhu Hassan katika mkutano wao uliofanyika Agosti 10 mjini Chamwino, Dodoma. Mahojiano kamili yako kwenye chaneli yetu ya YouTube.
без подписи
️️➟ @HabariTz ✰✰✰ Cultural Center of the I.R. of Iran - Dar es Salaam | Dar es Salaam Mataifa kama Ufaransa hayana tena mamlaka ya kimaadili ya kuuhubiria ulimwengu kuhusu "haki za binadamu" na sheria za kimataifa. Unafiki wao umefikia kikomo. Kuunga mkono vitendo vya kikatili dhidi ya Gaza na uchokozi dhidi ya Iran kumefuta kabisa kile walichokiita "msimamo wa kimaadili." Wakati umefika kwa ulimwengu kuona ukweli halisi, sio hotuba zao tupu. Dr. Abbas Araghchi, Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran
️️➟ @HabariTz ✰✰✰ BBC News Swahili Baada ya kuahirishwa kwa shauri la uhaini linalo mkabili Mwenyekiti wa Chadema Tundu Lissu, Katibu mkuu wa Chama hicho John Mnyika amewataka wapenzi na wafuasi wa chama hicho kuhuduria kwa wingi mahakamani siku ya Jumatatu kwani dakika za mwisho kwa upande wa mashitaka kuwasilisha ushahidi wao. Mnyika amekwenda mbali zaidi pia kwa kulitaka jeshi la polisi kushika doria bila ya kuwabugudhi wafauasi wao watakaojitokeza mahakamani hapo siku hiyo - - 📹 @eagansalla_gifted_sounds
️️➟ @HabariTz ✰✰✰ BBC News Swahili Jiunge na chaneli ya WhatsApp ya BBC News Swahili kupokea habari kwa kubofya link kupitia Instagram Stories ya BBCSwahili - - -
без подписи
без подписи
без подписи
без подписи
без подписи
без подписи
️️➟ @HabariTz ✰✰✰ BBC News Swahili Kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, imehairishwa mpaka Jumatatu baada ya upande wa mashataka, kuomba Mahakama ihairishe kwa sababu shahidi wao amepata dharura. Siku ya Jumatatu upande wa Mashtaka wataleta mashahidi wao wote. - -
️️➟ @HabariTz ✰✰✰ BBC News Swahili Haaland anaendelea kuandika historia! ⚽ Kutoka kufikisha magoli 100 Premier League kwa kasi zaidi hadi kufunga magoli matano katika mchezo mmoja wa Champions League mshambuliaji huyo wa Norway tayari ameweka rekodi kadhaa kubwa. Je, unazijua zote? Mwandishi wa BBC @loko_omi na taarifa zaidi - -
️️➟ @HabariTz ✰✰✰ Shahidi ashindwa kutokea, Lissu ashusha vifungu hivyo hivyo Kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu, imeahirishwa leo, Agosti 14, 2026, hadi Agosti 17, 2026. Hatua hiyo imekuja kufuatia ombi la upande wa Jamhuri kuomba ahirisho kutokana na dharura ya kiafya iliyompata shahidi wao hivyo kumfanya awepo Muhimbili. Pamoja na taarifa hiyo, Lissu aliamua kutumia muda huo kuishawishi Mahakama isikubali suala hilo kwa kutumia kesi mbalimbali za nyuma.
️️➟ @HabariTz ✰✰✰ 'Mkipata nafasi msaidieni mke wangu',Mhadhiri UDOM anayeshitakiwa kesi ya ugaidi
️️➟ @HabariTz ✰✰✰ Wakazi wa Kiembeni-Kibaha Mjini, kuchimbiwa kisima cha maji Hali ya maisha ya wakazi wa Kiembeni, Kibaha Mjini, inategemewa kubadilika, baada ya serikali kuanzisha uchimbaji kisima katika eneo hilo ukiwa ni mpango wa muda mfupi. Mnamo Agosti 11, 2026, wakazi wa eneo hilo waliongozana mpaka ofisi za Kata, kueleza malalamiko yao ikiwemo kupata magonjwa ya mara kwa mara kutokana na kutumia maji yasiyo salama, hasa hasa maji kutoka katika madimbwi na visima bubu. "Tuna furaha kubwa sana wana kiembeni maana tulikuwa tumechoka kukesha usiku tunakesha saa nane za usiku tunaacha vitanda, tunaacha wa watoto wamelala tunakuja kulindia maji," ameeleza Neema Lutumu, ambaye alikuwa ni mmoja wa wananchi waliowasilisha kero hiyo ofisi za kata.
️️➟ @HabariTz ✰✰✰ DW Kiswahili Marekani inamshinikiza Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu kulaani hadharani mzingiro unaofanywa na walowezi wa Kiyahudi katika kijiji cha Wapalestina cha Qusra, kilicho katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu na Israel. Umoja wa Mataifa unasema Wapalestina 15, wakiwemo watoto wawili, wamekwama majumbani mwao bila maji wala umeme
️️➟ @HabariTz ✰✰✰ DW Kiswahili Viongozi wa Mila wa Shomoo wametoa onyo kali kwa wanaodaiwa kuwa na nia ovu dhidi ya Rais Samia Suluhu Hassan na Dkt. Hussein Mwinyi, wakitangaza mpango wa kuweka sega la nyuki katika Ikulu za Dodoma na Zanzibar. Je, hatua hii ina ujumbe gani kwa wale wenye nia ovu dhidi ya viongozi hao? #dwKiswahili
️️➟ @HabariTz ✰✰✰ DW Kiswahili Zambia imesitisha zoezi la kuhesabu kura kote nchini leo Ijumaa kufuatia ripoti za vurugu katika baadhi ya maeneo. Afisa mkuu wa uchaguzi Brown Kasaro amesema "Ghasia hizo zinawalenga wafanyakazi wa uchaguzi, na katika baadhi ya matukio zimesababisha wizi wa karatasi za kura kwenye masanduku ya kura". Ameongeza kuwa tume hiyo itatathmini upya uamuzi wa kusitishwa zoezi hilo ndani ya saa 24. Taifa hilo lenye utajiri wa shaba kusini mwa Afrika lilipiga kura Alhamisi katika uchaguzi ulioangazia zaidi hali ngumu ya kiuchumi. Rais Hakainde Hichilema, ambaye amekuwa madarakani tangu 2021, alikabiliana na Brian Mundubile, waziri wa zamani mwenye umri wa miaka 55 katika serikali iliyopita ya Patriotic Front (PF). Mundubile amedai kushinda, huku Hichilema akisema timu yake inapokea "matokeo ya kutia moyo".