Infinite Kiumeni
СтатистикаJIFUNZE. Kumtongoza Mwanamke Unayempenda, Kumpata na Kuwa Naye Kimahusiano, Kudumisha Mahusiano na Ndoa, Kuongeza Nguvu za Kiume, Kumridhisha Kitandani, Maneno Matamu ya Kumsifia na Kumfanya Mwanamke Akupende Zaidi, Kumrudisha Ex Wako.
- Последний пост
- 10 мар.
- Последнее чтение
- 13 авг.
- Постов за неделю
- 0
- Всего постов
- 20
- Тип
- открытый
- Язык
- zu
- В каталоге с
- 13 авг.
- 1/24сутки в ленте
- —
- 1/48двое суток
- —
- 1/72трое суток
- —
Оценка по просмотрам недавних постов: пост набирает почти всё за первые сутки.
Посты
Usijilinganishe na mtu mwingine Usimlinganishe mke wako na mke wa mwingine. Jivunie uliyenaye na ambaye umepanga kujenga naye maisha. Mlinganishe maisha yake ya sasa na mwaka uliopita. Na sio umlinganishe na mwanamke mwingine nje.
Usimpe mwanamke uhuru kupitiliza. Lazima umfanye aone yupo chini ya utawala fulani na sio kama vile yupo kivyake. Usimmbane kupitiliza lakini asijione yupo huru sana. Lazima awe na uoga fulani na awe na kitu cha kupoteza. Japo unaweza kuambia mwache na uhuru wake lakini usifanye hivyo, utaumia.
Changamoto inapoteza ugumu wake pale unapoitatua. Mechi tamu inapoteza utamu wake wa mwanzo ukishaiangalia. Muvi nzuri inapoteza ule uzuri wa mwanzo ukishaiangalia. Na baada ya muda inaboa na unapotezea maisha yanasonga. Hata wewe ukipoteza uongozi wako utakuwa unaboa. Na mwanamke ataona hana ile raha ya kukaa na wewe tena Ataondoka na maisha mengine yataendelea.
Ukitaka kufaidi mahusiano, usitake yawe yakikamilifu Kubali mapungufu yalipo. Lakini, usikubali maudhi na makusudi. Hivyo, tambua tofauti ya mapungufu na makuzi/ maudhi/ makusudi/ tabia zisizofaa. Mapungufu unaweza kuvumilia, ila hivyo vingine si vya kuvumilia.
Anza mwezi kwa nguvu mpya. Bila kujalisha ulimalizaje mwezi uliopita, uchukulie huu mwezi mpya na upya wake. Vilivyokukwaza mwezi uliopita, usiende navyo mwezi huu. Na usikate tamaa.
Kuishi maisha magumu ni maamuzi. Kwasababu, maisha hayana ugumu wala urahisi bali yana changamoto. Maisha yana vipindi, vya shida na raha. Na unaweza kuamua maisha yako yaweje katika hivyo vipindi. Na ukisema maisha magumu basi umechagua mwenyewe yawe hivyo.
Kiongozi, kumbuka kwamba Mwanamke ataendelea kuwa kwenye maisha yako kwasababu ya uongozi wako imara. Utakapoonesha udhaifu utaona na yeye anaonesha dalili za kujitoa kwenye maisha yako. Jikumbushe kurudi kwenye uimara wako.
Punguza kulaumu watu Punguza kutoa lawama Bali tafuta suluhisho. Hata kwa vitu vidogo, Jizoeshe kutafuta suluhisho. Hii itakusaidia kupunguza stress. Utapata usingizi mzuri, na utakuwa na afya.
Kuwa makini na historia ya mwanamke. Wanawake wengi wakitaka kuolewa ndiyo wanakimbilia dini ili waonekane wasafi Lakini walipokuwa hawana lengo la kuolewa waliweka dini pembeni. Hii ndiyo sababu tunafundishwa kuoa mwanamke bikra, Ili umjenge wewe na umuongoze kirahisi.
Usikate tamaa. Kama rafiki yako amekutenga, jipandishe hadhi upate marafiki wapya wanaoendana na wewe. Kama mwanamke amekuacha. Jiendeleze na uvutie mwanamke wa hadhi yako. Kama umepoteza hela/ kazi/ biashara. Kaa chini utafakari, uongeze ujuzi na uanze tena kwa kujifunza. Lakini, usikate tamaa. Usilalamike kila saa, wala usipoteze muda kuishi kwenye unyonge. Simama tena!
Njia mojawapo anayotumia mwanamke kumrubuni mwanaume ni kumuonesha urafiki wakati amemkataa kimapenzi. Unaongea naye vizuri, lakini ukiweka mambo ya mapenzi/ mahusiano anakwepa kwepa. Ila anajifanya bado ni rafiki yako ili aendelee kula hela zako, au kukutumia kwa anavyojua yeye. Kama umekubali kuishi naye kama rafiki ni sawa, Lakini, kama unamtaka kimapenzi basi usikubali hiyo hali. Kata mawasiliano na ufanye mambo yako mengine.
Kiongozi usiogope kufanya makosa katika kujiendeleza kimaisha. Ukiachana na makosa makubwa yatakayokupa hasara kubwa kama vile kufungwa jela, au kupata ulemavu, basi makosa mengine unaweza kufanya. Katika safari yako ya kujiendeleza utajikuta tu unafanya makosa kwenye maamuzi yako. Unapaswa kujifunza kutokana na hayo makosa. Usipoteze muda mwingi kujilaumu, bali tafuta suluhisho na usonge mbele.
Kufanya sex mara kwa mara itakusaidia kudumu muda mrefu kwenye tendo. Kwasababu utapata uzoefu zaidi wa kujua ufanye nini muda gani ili usimwage haraka. Practice makes perfect. Unavyofanya jambo fulani ndivyo unakuwa vizuri zaidi kwenye hilo jambo. Na ufanye kwa ufasaha ili upate uzoefu mzuri.
Kufanikiwa = Kushindwa bila kukata tamaa. Yaani, kadri unavyoinuka tena baada ya kukwama, ndivyo unajiongezea nafasi ya kushinda. Kushinda sio muujiza, na haitokei tu. Kushinda ni hatua. Kwahiyo, usikate tamaa popote ulipo kwenye malengo yako. Endelea kusonga mbele.
Anza wiki yako kwa kuendelea kufikia malengo yako. Anza wiki kwa lengo la kupata pesa zaidi. Usiogope pesa. Usiseme pesa sio ya muhimu/ sio kila kitu. Wewe ongeza kipato chako. Endelea kuongeza pesa nyingi kwa kadri ya uwezo wako. Usijiwekee kikomo. Pesa ni ya MUHIMU, usiogope kuwa nazo.
Kwenye siku hii ya wapendanao, onesha kujali watu wako wa karibu. Wajulie hali watu wako wa karibu na familia. Sio kwa mpenzi wako tu.
Ukiachana na wanawake wasio na mpango na wewe itakusaidia sana. Utapunguza stress, Utapunguza matumizi ya hela yasiyo ya lazima. Usilazimishe sana kwa mwanamke asiyeonesha mwelekeo kwako. Na kama huwa unakutana na wanawake aina hiyo tu, basi badilisha Thamani yako. Ongeza Thamani yako.
Upendo wa mwanamke kwa ndugu ni tofauti na upendo wake kwa mpenzi. Upendo wake kwa kaka yake ni tofauti na kwa mume wake. Kwahiyo, kama una lengo la kupata upendo wa mapenzi, Basi usikubali kupewa upendo wa kikaka.
Kutoishi kwenye malengo yako ni chanzo kimojawapo cha sisi wanaume kuwa na huzuni Utajikuta unakosa furaha na una majuto mengi. Lakini, ukiishi kwenye malengo yako na ukiwa unayafikiria mara kwa mara utakuwa na furaha. Hali ya huzuni, kushindwa, kuogopa zitapungua sana. Na utaishi maisha ambayo mara nyingi una furaha.
Ukiwa na pesa ina faida nyingi kama vile - Unaweza kuchagua marafiki unaotaka - Ukaacha kazi usiyoipenda - Ukaendesha mahusiano unavyotaka - Ukaendesha maisha yako unavyotaka Na fursa ni nyingi zaidi ukiwa na pesa. Kwahiyo, tuhakikishe tunachuma pesa nyingi kadri iwezekanavyo. Achana na misemo kama pesa si kitu/ kila kitu. Au, pesa ni chanzo cha maovu Bali angalia maisha unayotaka yanahitaji nini. Na utambue pesa ni muhimu hata kama unaiona ni mbaya.