tgindex
Isaack Nsumba

Expert & Competent Teacher In Love, Relationship and Marriage.

Последний пост
20 февр.
Последнее чтение
01:24
Постов за неделю
0
Всего постов
116
Тип
открытый
Язык
английский
Категория
Новости и СМИ (по похожим)
В каталоге с
13 авг.
Подписчики
4 536
−26 за 4 дн.
Сутки
−6
−0,13%
Неделя
 
Месяц
 
Просмотров на пост
1 978
40 постов
Вовлечённость
43,6%
к подписчикам
Постов в день
0,0
всего 116
Упоминаний
0
каналов
Охват размещения
оценка
1/24сутки в ленте
1/48двое суток
1/72трое суток

Оценка по просмотрам недавних постов: пост набирает почти всё за первые сутки.

Посты

  • 20 февр.1 62114

    Aina 2 Za Mawasiliano Wakati Wa Mgogoro Katika Mahusiano — Ni Aina Ipi Mnaitumia Mara Kwa Mara? Mahusiano mengi hayavunjiki kwa sababu ya kukosa mapenzi, bali kwa sababu ya jinsi watu wanavyozungumza wanapokuwa na maumivu, hasira au kutokuelewana. Maneno tunayochagua, sauti tunayotumia, na namna tunavyojieleza wakati wa mgogoro vinaweza kujenga daraja la uelewano au kubomoa kabisa uhusiano. Ndani ya mahusiano, kuna aina mbili kuu za mawasiliano zinazotawala—moja huongeza migogoro, na nyingine hutatua migogoro. Aina unayotumia mara kwa mara ndiyo huamua kama mtaendelea kukua pamoja au kuumizana taratibu bila kujua. Hebu tuziangalie kwa kina. 1. Aggressive Communication (Mawasiliano ya Kivita/Ukali) Hii ni aina ya mawasiliano ambayo mtu, Anataka kutawala mazungumzo, Anaamini lazima ashinde, hata kama mwenzake anaumia Hachukulii hisia za mwenzake kama kitu cha maana Dalili zake: Sauti ya juu au ya kejeli, Lawama za moja kwa moja (“Wewe ndio shida”) Kudharau, matusi, vitisho au dharau za kimya kimya, Kukatisha mwenzake anapoongea Nk Athari kwenye mahusiano Zinaweza Kuwa, Huua usalama wa kihisia, Husababisha mwenzake kujifunga au kulipiza kisasi, Migogoro huongezeka badala ya kupungua, Mapenzi hugeuka mashindano ya nani ana nguvu zaidi Kimsingi, Aggressive communication hujenga hofu, si upendo. 2. Assertive Communication (Mawasiliano ya Ukomavu) Hii ni aina ya mawasiliano ambapo mtu, Anajithamini na anamthamini mwenzake, Husema ukweli bila kuumiza, Analenga suluhisho, sio lawama Dalili zake: Sauti ya utulivu hata ukiwa umeumia, Kutumia “Ninajisikia…” badala ya “Wewe kila mara…Kusikiliza bila kukatisha, Kuonyesha mipaka bila ugomvi Athari kwenye mahusiano: Huongeza uaminifu, Hujenga usalama wa kihisia, Hufanya migogoro kuwa daraja, sio ukuta, Huwezesha mapenzi kukua kwa Urahisi. Swali: Wewe Huwa Unatumia Aina Ipi Ya Mawasiliano? Mwenzi Wako Nayeye Anatumia Aina Ipi? By The Way, Kama Umeipenda Makala Hii Follow Page Hii Kwa Ajili Ya Mafunzo Zaidi: @IsaackNsumba @IsaackNsumba @IsaackNsumba @IsaackNsumba @IsaackNsumba #Mapenzi #Mahusiano #DarEsSalaam #Tanzania #Uchumba #Ndoa

  • 16 янв.2 4865

    0749 972 733

  • 26 окт.4 07034

    Ulimtaka Alipokuwa Binti Mdogo, Akakukataa. Hivi Sasa Amekuwa Mtu Mzima, Soko Limemkataa Ndo Amerudi Kwako... Kumpokea Ni Udhaifu. Ulipokuwa Hauna Kitu Hakuwahi Kuonesha Kuvutiwa Nawewe, Hivi Sasa Una Vyako Ndo Anakuonesha "You Mean Everyrhing To Her" Kumpokea Ni Udhaifu Mkubwa. Uliwahi Kumtaka Kipindi Hana Mtoto Hata Mmoja, Akakupuuza. Amekwenda Dunia Imemuharibu, Kazalishwa Na Kutelekezwa Ndipo Anakuja Kwako. Kumpokea Ni Ujinga. Kwa Wanaume Wengine Alikuwa "ANA BUY TIME" Ila Kwako Anataka Ndoa. Ukimuoa Wewe Ni Mjinga. Mwanamke Ambae Hakuwahi Iamini Kesho Yako, Leo Anataka Usijali Kuhusu Past Yake Ukikubali We Ni Bwege. Bro, Fanya Uwezavyo...Dont Be Her Retiring Plan.

  • Jaza Fomu Hii, Kama UNAHITAJI KUPATA MWENZA >>>https://forms.gle/UZw8pyEnJMzSJ9FE9

  • Kama Unahitaji Kujifunza Kupitia VIDEO ZANGU, Subscribe Katika Channel Yangu Ya Youtube >>>https://www.youtube.com/@isaacknsumba

  • Maumivu Hayataondoka Kama Unafanya Haya 4... 1. Kuyakataa au Kuyakimbia Maumivu yanahitaji kukubaliwa kabla ya kuponywa. Unapokataa Au Unapojaribu Kuyakimbia Yatakutesa Sana! Fungua Moyo Wako, Kubali Kuwa Kuna Maumivu Unayapitia. Kukubali Ni Hatua Muhimu Sana Katika Kukabiliana Nayo. 2. Kuendelea Kumfuatilia Kushikilia yaliyopita hukuzuia kuendelea mbele. Hautakiwi Kuendelea Kumfuatilia Uliyeachana Nae. Kubali Kwamba Sio Wako Tena Na Usonge Mbele. 3. Kutumia Kilevi Njia Hii Hupunguza hisia kwa muda tu, lakini huongeza mateso ya baadaye. Pombe Hukulaghai, Na Kukufanya Ujione zuko Sawa. Ikiisha Unakuta Tatizo Liko Palepale...Manake Utalazimika Kunywa Tena Ili Usiliface. 4. Kuanzisha Uhusiano Mpya Haraka Hii Inaweza Kuonekana Njia Inayofaa, Lakini Ni kujificha, siyo uponyaji. Mimi Sishauri Uanzishe Mahusiano Mapya Mara Baada Ya Kuachwa Au Kuachika. Kwa Sababu Sio Njia Salama Ya Kushufhulikia Maumivu. Badala yake, kubali maumivu, tafuta msaada, na jipe muda wa kupona. By The Way, Kama Umeipenda Makala Hii Follow Page Hii Kwa Ajili Ya Mafunzo Zaidi: @IsaackNsumba #Mapenzi #Mahusiano #DarEsSalaam #Tanzania #Uchumba

  • Kama Unahitaji Kujifunza Kupitia VIDEO ZANGU, Subscribe Katika Channel Yangu Ya Youtube >>>https://www.youtube.com/@isaacknsumba

  • Usikubali Kumpoteza Mwanamke Mwenye Sifa Hizi 4... 1. Ambae Anakuongelesha Vizuri HATA AKIWA NA HASIRA. Wanawake Wengi Ni VIUMBE WA HISIA, Wengi Hawawezi Kucontrol Hisia Zao. Ndio Maana Wakikasirika Wanaropoka. Ukimpata Ambae, Hata Kama Umemkasirisha Bado Anaweza KUKUONGELESHA KWA HESHIMA, Mtunze Huyo. 2. Ambae Anajali Na Kuzingatia FURAHA YAKO. Wanawake Wengi Ni WABINAFSI SANA, Wengi Wapo Upande Wa KUFANYIWA na KUPOKEA. Wanajali Na Kuzingatia Furaha Zao Na Kusahau Za Wanaume Zao. Kama Unae Ambae ANAJITAHIDI KUKUFANYA UFURAHI, Anajali Na Kuzingatia Furaha Yako, Weka Pete Kidoleni Kisha Mzalishe Watoto 3. 3. Ambae Anaweza Kutumia FEDHA YAKE KWAAJILI YAKO. Wanawake Wamejiwekea Ukuta Kati Yao Na Wanaume Zao Linapokuja Suala la Fedha. Huwa Wanaona Kama Fedha Zao Ni Za Kwao Pekeyao. Ndio Maana, Mwanaume Anaweza Pitia Kipindi Kigumu Na Asipate Backup Kutoka Kwa Mwanamke Wake. Kama Uliyenae Anaweza Kutumia Fedha Zake Kwaajili Yako, Umepata Mwanamke Mzuri Mzee. 4. Anaeyajua Madhaifu Yako Na BADO AMESIMAMA NAWEWE. Wapo Wanaume Wengi Sana Ambao Wamekimbiwa Na Wanawake Zao, Kisa Udhaifu Huohuo Ulionao Wewe. Na Pengine Udhaifu Ambao Wengine Walishindwa Kuuvumilia Yeye Ameweza. Mwanamke Kama Huyo Usikubali Kumpoteza. Anafaa Kuitwa Kwa Ubini Wako, Nenda Kwao Haraka Sana! Mkitoka Mpeleke Kwa Baba Na Mama, Kisha Muweke Ndani Mfanye Maisha. By The Way, Kama Umeipenda Makala Hii Follow Page Hii Kwa Ajili Ya Mafunzo Zaidi: @IsaackNsumba #Mapenzi #Mahusiano #DarEsSalaam #Tanzania #Uchumba #Ndoa

  • Sikiliza Hapa Speech Niliyotoa Baada Ya Kukabidhiwa Tuzo Ya Mtaalam Wa Mahusiano >>>https://youtu.be/8w0MFYjyRt0?si=OrGNwbKv770DecOZ

  • Mambo 4 Ya Kufanya, UKIGUNDUA UNAEMPENDA HAKUPENDI.... 1. Kubali Ukweli Mchungu (Accept The Bitter Truth) Hatua Ya Kwanza Ya Kupata Amani Ni Kukubali Hali Halisi. Kumbuka, Kutojali Au Kujaribu Kubadilisha Hisia Za Mwengine Hakutasaidia. Kukubali Kweli Kunakusaidia Kuacha Kuumiza Moyo Wako Na Kuanza Kuponya. Lakini Pia Kutakusaidia Kusitisha Uwekezaji Wako Kwake (Wa Muda, Fedha Na Hisia) 2. Tengeneza Umbali (Create Distance) Kuendelea Kuwa Karibu Na Mtu Anayechezea Na Kupuuza Hisia Zako Kunaleta Huzuni Na Kujiona Haufai. Tengeneza Umbali Wa Kimwili Na Kihisia Ili Kupunguza Maumivu. Hii Inaweza Kujumuisha Kupunguza Mawasiliano, Kuepuka Kukutana Mara Kwa Mara, Au Kuweka Mipaka Wazi. 3. Futa Kumbukumbu (Delete Memories) Si Lazima Kuondoa Kila Kitu, Lakini Fanya Jitihada Kupunguza Kumbukumbu Zinazokuchochea Maumivu. Hii Inaweza Kuwa Kuondoa Picha, Kuacha Kumfuatilia Kwenye Mitandao Ya Kijamii, Au Kutozungumza Kuhusu Yeye. Lengo Ni Kuacha Kuishi Kwenye Yaliyopita Na Kuruhusu Moyo Wako Kupona Na Kusonga Mbele. 4. Fungua Moyo Kwa Anaekupenda (Open Your Heart To Someone Who Loves You) Baada Ya Kupona, Fanya Jitihada Kuona Na Kuthamini Wale Wanaokupenda Kwa Dhati. Usilazimishe Upendo Uliopotea; Badala Yake, Toa Nafasi Kwa Upendo Halisi Na Wenye Afya. Hii Ni Hatua Ya Kuanza Upya Na Kujenga Uhusiano Wenye Furaha Na Wenye Manufaa. Siku Utayompa Nafasi Anaekupenda Ndipo Utajua Mapenzi Sio Mabaya, Ni Vile Huwa Tunawapa Mioyo Yetu Watu Wasio Sahihi... Ambao Huishia Kutuumiza. By The Way, Kama Umeipenda Makala Hii Follow Page Hii Kwa Ajili Ya Mafunzo Zaidi: @IsaackNsumba #Mapenzi #Mahusiano #DarEsSalaam #Tanzania #Uchumba #Ndoa

  • Jinsi Ya Kufufua, Kuchochea Au Kuhuisha Penzi Lililopooza... Biblia Inasema "Msiyachochee Mapenzi, Wala KUYAAMSHA..." (Wimbo Ulio Bora 2:7) Biblia Isingesema "Msiyachochee" Kama Upendo Hauwezi Kuzima, Wala Iaingesema "Kuyaamsha" Kama Upendo Hauna Tabia Ya Kufifia, Kupooza N.k Kwahiyo Kumbe, Upendo Unaweza Kupooza, Kufifia, Kutoweka, Kufa... Na Unaweza Kuhuishwa, Kuchochewa na Ukaamka Tena. Hizi Ni Hatua Za Mchakato Wa Kuchochea Au Kuhuisha Penzi Lililopooza Ambao Kitaalam Huitwa "LOVE RESTORATION PROCESS" 1. Izungumzieni Hali Mnayopitia (Address The Issue Together) Kila Mmoja Anatakiwa Kuonesha Kuwa Hapendi hali Inayoendelea Katikati Yenu. Nyoote Kwa Pamoja Mnatakiwa Mzungumzie Sababu Za Hiyo Hali. Kama Ni Majeraha Ponyaneni, Kama Ni Makosa Ombaneni Msamaha. 2. Love Acts (Matendo Ya Kimapenzi) Fanyeni Matendo Yoote Yakimapenzi, Matendo Ambayo Yatairudisha Ile Emotional Link Iliyokuwepo Kati Yenu. Hapa Nazungumzia Kushikanashikana, Kupeana Zawadi, Kushiriki Tendo Nk. 3. Rejesheni Mawasiliano Ya Mara Kwa Mara Na Ya Kina. Kufufua Penzi Kunahitaji Kufufua Mawasiliano. Kwa Sababu Penzi Linapoanza Kupooza Eneo La Kwanza Kuashirika ni Mawasiliano. Mnatakiwa Kuwasiliane Kadri Muwezavyo, Tena Katika Levels Zoote 3, Yaani Superficial, Personal & Intimate Level. 4. Husisheni Nguvu Ya Kiroho (Spiritual Power) Nyuma Ya Kuvunjika Kwa Mahusiano Na Ndoa Nyingi (Sijasema Zoote) Kuna Vyanzo Vya Kiroho. Na Ikiwa Hivyo Hata Ufanyie Kazi Mbinu Nilizokufundisha Hautapata Matokeo. Hivyo Kuna Umuhimu Mkubwa Sana Kuhusisha Nguvu na Mikakati Ya Kiroho Kutatua Changamoto. Natamani Kupokea Ushuhuda Wako Baada Ya Kuyafanyia Kazi Haya. By The Way, Kama Umeipenda Makala Hii Follow Page Hii Kwa Ajili Ya Mafunzo Zaidi: @IsaackNsumba #Mapenzi #Mahusiano #DarEsSalaam #Tanzania #Uchumba #Ndoa

  • Mambo 7 Yanayojulisha Bado Unampenda Ex Wako na UNATAMANI KURUDIANA NAE... 1. Kumfuatilia Kisirisiri Unajikuta Unaangalia Status Zake, Profile, Au Kuuliza Kwa Marafiki Zake Bila Yeye Kujua. Unataka Kujua Kuhusu Yeye Na Maisha Yake Kiujumla. 2. Shauku Ya Kuwasiliana Naye Kila Mara Unashawishika Kumpigia Simu Au Kutuma Meseji, Hata Kama Unajizuia. Na Unaweza Jifanya Kama Umekosea, Au Kutuma Meseji Za Kichokozi, Kuuliza Maswali Nk. 3. Unatamani Kusikia Mabaya Yamempata Katika Mahusiano Yake Ndani Ya Nafsi Yako Unahisi Furaha Kidogo Kusikia Mambo Yake Mapya Hayamnyokei. Na Unatamani Mapenzi Yampige Kwelikweli Ili Ajutie Na Akukumbuke. 4. Unajilazimisha Furaha, Na Unataka Akuone Una Furaha Unajilazimisha Kumfanya Aone Kama Haumfikirii, Umeshamsahau Na Kumove On. Unapost Vitu Vya Kuonyesha Maisha Mazuri, Lakini Ndani Bado Unamuwaza. 5. Kutamani Kujua Kama Bado Anakupenda Au Amekumiss Unabaki Na Maswali Moyoni Kama Bado Anakufikiria. Unatamani Kujua Anawaza Nini Kuhusu Wewe, Unatamani Kujua Jinsi Anavyozungumza Kuhusu Wewe Huko Aliko. 6. Kusikia Maumivu Au Wivu Ukijua Ana Mtu Mwingine Habari Ya Yeye Kuwa Na Mwingine Inakuumiza Zaidi Ya Kawaida. Japo Kwa Nje Unaweza Kuonesha Kuwa Sio Habari Inayokugusa, Ila Ndani Inakusumbua Sana! 7. Kutunza Kumbukumbu Zake Hii Hujumuisha Picha, Zawadi Zoote Alizowahi Kukupa, Nfuo Zake Zilizobaki Kwako N.k Hiki Ni Kiashiria Tosha Kuthibitisha Kwamba Bado Anaishi Ndani ya Moyo Wako. Katika Makala Zijazo Nitakusaidia Jinsi Ya Kumrudisha Ex Wako Kirahisi Mno. Ila Leo Nambie, Katika Ya Hayo Mambo 6 Ni Jambo Gani Linakuhusu Moja Kwa Moja? By The Way, Kama Umeipenda Makala Hii Follow Page Hii Kwa Ajili Ya Mafunzo Zaidi: @IsaackNsumba #Mapenzi #Mahusiano #DarEsSalaam #Tanzania #Uchumba #Ndoa

  • Jinsi Ya Kukabiliana na Hali Ya KUKATA TAMAA Ya Kupendwa na Kupenda Tena... Makala Hii Inalenga Kumsaidia Mtu Ambae Amekata Tamaa Ya Kupenda na Kupendwa Tena Yaani Ni Maalum Kwa Mtu Ambae Amependa Mara Kadhaa Na Kuishia Kuumizwa. Na Akafika Hatua Ya Kuhitimisha "Hakuna Ambae Atanipenda Au Kuthamini Upendo Wangu Kwake" 1. Usihitimishe Kwamba MAPENZI YA KWELI HAKUNA. Mara Nyingi Hii Huwa Inatokea Tunapopenda Mara Kadhaa na Kuishia Kuumizwa. Tunaamini Hakuna Mapenzi, Hakuna Ambae Anaweza Akaja Kuthamini Upendo Wetu. Jitahidi Sana Usifike Hiyo Level, Amini Kwamba Mapenzi Mazuri Yapo, Amini Kwamba Watu Wazuri Wapo Ila Ni Haujakutana Nao Bado. Watu Wachache Waliokutenda Wasifanye Ushindwe Kuwapa Nafasi Watu Wazuri. Mapenzi Ya Kweli Wapo, Ni Vile Unakutana Na Watu Wabaya. 2. Yape Mapenzi NAFASI NYINGINE TENA. Wapo Watu Ambao Waliumizwa Mara Kadhaa Na Kutamani Kukata Tamaa. Wakasema "Ngoja Nijaribu Kwa Mara Nyingine" Ndipo Muujiza Wao Ulitokea. Walipendwa na Kuthaminiwa na Wakasahau Maumivu Yooote Ya Nyuma. Nashauri Nawewe Ufanye Hivyo, Usiyakatie Tamaa Mapenzi. Yape Nafasi Nyingine Tena. Nina Ushuhuda Wa Waliokuwa Wamekaribia Kukata Tamaa Kama Wewe, Walipojaribu Tena na Tena Mambo Yalibadilika. Walifutwa Machozi Na Kuoneshwa Thamani Yao Halisi, Nakuombea Imawe Hivyo Kwako Pia. By The Way, Kama Umeipenda Makala Hii Follow Page Hii Kwa Ajili Ya Mafunzo Zaidi: @IsaackNsumba #Mapenzi #Mahusiano #DarEsSalaam #Tanzania #Uchumba #Ndoa

  • OFFER NDANI YA MASAA 6 TU! Wrngi Mmekuwa Mkitamani Kupata Dawa Kutoka NSUMBA HERBAL CLINIC. Kimsingi, Dawa Zetu Huwa Tunauza Dozi 200,000 Nusu 100,000. Ila Ukilipia BIGPEN LEO Ndani Ya Masaa 6 Kutoka Sasa. Tutakusaidia Dozi Kwa 180,000 Na Nusu Dozi Kwa 90,000. Na Utafanyiwa FREE DELIVERY. Clinic Yetu Ipo Dar Es Salaam, Mawasiliano Stend (Geti La Kutokea) Kuna Ghorofa Yenye ATM Ya CRDB & NMB. Juu Ghorofani Ndipo Ofisi Ilipo Na Jina La Ofisi Ni; NSUMBA HERBAL CLINIC. Kwa Maelezo Zaidi Unaweza Kutupigia Kwa Namba; 0749 972 733 0768 544 615 0682 917 370 Nsumba Herbal Clinic "Priotize Your Health, Your Life Matters"

  • Wanawake Wana Changamoto Sana Lakini MWENYE SIFA HIZI USIMUACHE. 1. Ambae Anakuongelesha Vizuri HATA AKIWA NA HASIRA. Wanawake Wengi Ni VIUMBE WA HISIA, Wengi Hawawezi Kucontrol Hisia Zao. Ndio Maana Wakikasirika Wanaropoka. Ukimpata Ambae, Hata Kama Umemkasirisha Bado Anaweza KUKUONGELESHA KWA HESHIMA, Mtunze Huyo. 2. Ambae Anajali Na Kuzingatia FURAHA YAKO. Wanawake Wengi Ni WABINAFSI SANA, Wengi Wapo Upande Wa KUFANYIWA na KUPOKEA. Wanajali Na Kuzingatia Furaha Zao Na Kusahau Za Wanaume Zao. Kama Unae Ambae ANAJITAHIDI KUKUFANYA UFURAHI, Anajali Na Kuzingatia Furaha Yako, Weka Pete Kidoleni Kisha Mzalishe Watoto 3. 3. Ambae Anaweza Kutumia FEDHA YAKE KWAAJILI YAKO. Wanawake Wamejiwekea Ukuta Kati Yao Na Wanaume Zao Linapokuja Suala la Fedha. Huwa Wanaona Kama Fedha Zao Ni Za Kwao Pekeyao. Ndio Maana, Mwanaume Anaweza Pitia Kipindi Kigumu Na Asipate Backup Kutoka Kwa Mwanamke Wake. Kama Uliyenae Anaweza Kutumia Fedha Zake Kwaajili Yako, Umepata Mwanamke Mzuri Mzee. 4. Anaeyajua Madhaifu Yako Na BADO AMESIMAMA NAWEWE. Wapo Wanaume Wengi Sana Ambao Wamekimbiwa Na Wanawake Zao, Kisa Udhaifu Huohuo Ulionao Wewe. Na Pengine Udhaifu Ambao Wengine Walishindwa Kuuvumilia Yeye Ameweza. Mwanamke Kama Huyo Usikubali Kumpoteza. Anafaa Kuitwa Kwa Ubini Wako, Nenda Kwao Haraka Sana! Mkitoka Mpeleke Kwa Baba Na Mama, Kisha Muweke Ndani Mfanye Maisha. By The Way, Kama Umeipenda Makala Hii Fanya Haya: 1. Comment Kitu Ulichojifunza 2. Follow Page Hii Kwa Ajili Ya Mafunzo Zaidi 3. Save Post Hii Kwa Matumizi Ya Baadaye 4. Share Post Hii Ili Iwasaidie Wengine Wengi Isaack Nsumba #Mapenzi #Mahusiano #DarEsSalaam #Tanzania #Uchumba #Ndoa

  • Awamu 6 Ambazo Mahusiano Hupita Hadi Kufikia Hatua Ya Kudumu... Awamu Ya KWANZA; The Dream Phase.. Hii Ni Hatua Ya Mwanzo Kabisa Ambapo Kila Mmoja Humtazama Mwenzie Katika Jicho la Ukamilifu. Kila Mmoja Huimagine Jinsi Maisha Yatakavyojaa Furaha Akiwa na Mwenzie. Awamu Ya PILI; The Discover Phase. Hapa Kila Mmoja Anaanza Kuona Madhaifu Ya Mwenzake Waziwazi. Yale Ambayo Yalikuwa Hayaonekani Katika Hatua Ya 1 Hapa Yanaonekana Waziwazi. Awamu Ya TATU; The Disapointment Phase. Baada Ya Kukutana na Kile Ambacho Hakutarajia, Kila Mmoja Huvunjika Moyo. Hapa Ndo Mtu Husema "Nilidhani Hivi, Kumbe Siovyo...Yuko Vile" Hapa Ndio Mtu Hugundua Uongo Woote na Mambo Kadhaa. Awamu Ya NNE; The Rebuilding Phase. Katika Hatua Hii Migogoro Yoote Inachukuliwa na Kutafutiwa Ufumbuzi. Hapa Mnaacha Kulumbana, Mnaanza Kuliumba na Kulijenga Upya Penzi Lenu. Hii Hatua Huwa Wanafika Wachache Sana! Awamu Ya TANO; The Deep Love Phase. Penzi Linazaliwa Upya, Kila Mmoja Amejifunza Kumpenda na Kumpokea Mwenzie Jinsi Alivyo. Hapa Ukomavu Wa Hisia Unahusika, Ambapo Kila Mmoja Hutambua Kuwa Hakuna Aliye Mkamilifu. Ukiwakuta Watu Katika hatua Hii, Ni Kama Penzi Limeanza Jana. Awamu Ya SITA; The Legacy Phase. Ni Katika Hatua Hii Ambapo Penzi Hugeuka na Kuwa La Kuigwa na Watu Wengine. Hapa Sasa Ndio Wengine Huanza Kusema "Hawa Wanapendana" Kila Ambae Anawajua Anaona Jinsi Penzi Lilivyoweza Kuwa Hai Licha Ya Kukumbana na Changamoto kadhaa. Mara Nyingi, Ni Asilimia Chache Sana Wanaofika Hatua Ya 6, Wengi Huachana Katika Hatua Ya 3. Mnahitaji Maarifa Yatakayowasaidia Kuvuka Hatua Ya 3 Ili Msiishie Hapo Kama Wengine. Je...Ndoa Yako Au Mahusiano Yako Yapo Hatua Gani Hivi Sasa? By The Way, Kama Umeipenda Makala Hii Fanya Haya: 1. Comment Kitu Ulichojifunza 2. Follow Page Hii Kwa Ajili Ya Mafunzo Zaidi 3. Save Post Hii Kwa Matumizi Ya Baadaye 4. Share Post Hii Ili Iwasaidie Wengine Wengi Isaack Nsumba #Mapenzi #Mahusiano #DarEsSalaam #Tanzania #Uchumba #Ndoa

  • Aina 4 Za Heshima (Kwa Ambae Anataka Jamii Imuheshimu) 1. Position Respect (Heshima Ya Nafasi/Madaraka) Hii Ni Heshima Inayotokana Na Cheo, Mamlaka Au Nafasi Ya Mtu Katika Jamii, Serikali Au Taasisi. Mfano: Rais, Mwalimu, Kiongozi Wa Dini, Au Bosi Kazini. Hata Kama Mtu Binafsi Hana Tabia Nzuri, Watu Wengi Bado Wanampa Heshima Kwa Sababu Ya Cheo Chake. Ni Heshima Inayoambatana Na Hofu Ya Walio Chini Yake. 2. Talent Respect (Heshima Ya Kipaji) Hii Hutokana Na Kipaji Cha Kipekee Alicho Nacho Mtu. Mfano: Msanii Mzuri Wa Muziki, Mchezaji Bora Wa Mpira, Au Mchoraji Maarufu. Watu Wanamthamini Kwa Kile Anachoweza Kufanya Tofauti Na Wengine. 3. Success Respect (Heshima Ya Mafanikio) Hii Hutokana Na Matokeo Ya Maisha, Mafanikio Ya Kifedha, Kielimu Au Kijamii. Mfano: Mfanyabiashara Aliyefanikisha Kampuni Kubwa, Mtu Aliyepata Utajiri, Au Mwanafunzi Aliyefaulu Sana. Heshima Hii Hujengwa Kwa Matokeo Yanayoonekana. 4. Expertise Respect (Heshima Ya Utaalamu) Heshima Hii Hutokana Na Ujuzi Maalum Au Maarifa Ya Kitaalamu Ambayo Mtu Anayo. Mfano: Daktari Bingwa, Injinia, Profesa, Au Fundi Mwenye Ujuzi Wa Hali Ya Juu. Watu Wanamheshimu Kwa Sababu Ya Uelewa Wake Wa Kitaalamu Na Mchango Wake Kwa Wengine. Je! Wewe Unajenga Aina Ipi Ya Heshima Kati Ya Hizo 4? By The Way, Kama Umeipenda Makala Hii Fanya Haya: 1. Comment Kitu Ulichojifunza 2. Follow Page Hii Kwa Ajili Ya Mafunzo Zaidi 3. Save Post Hii Kwa Matumizi Ya Baadaye 4. Share Post Hii Ili Iwasaidie Wengine Wengi Isaack Nsumba #Mapenzi #Mahusiano #DarEsSalaam #Tanzania #Uchumba #Ndoa

  • [VIDEO YOUTUBE]; Jinsi Ya Kufufua Penzi Lililopooza Au Lililokufa >>>https://youtu.be/YPNponL0AcU Ukishatazama Video, USISAHAU KUSUBSCRIBE

  • Wakati Mgumu Utakaokutana Nao Unapotaka Kuachana na Mtu. Wakati Mgumu Katika Mahusiano Ni Pale Ambapo UNATAKIWA KUACHANA NA MTU HUKU BADO UNAMPENDA. Ndio Wakati Pekee Ambapo Unaweza Kujikuta NJIA PANDA. Kuondoka Unaona Ni Uamuzi Mzuri Kabisa Na Kuendelea Bado Unataka. Katika Wakati Kama Huu Kuna Hisia Zitakuvamia Za Kuanza Kuhisi Kama KUNA KITU UNAPOTEZA. Katika Nyakati Kama Hivi Kuna Mambo 3 Natamani Uyajue. 1. Ni Kawaida KUENDELEA KUMPENDA (Its Ok To Still Love) Mtu Ambae Amekuwa Sehemu Ya Maisha Yako Ukawekeza Muda, Hisia na Energy Kwake HAIWEZI KUWA RAHISI KUACHANA NAE. Hivyo Ni Kawaida Kujihisi Bado Unampenda Mnapotaka Kuachana. 2. Ni Kawaida KUJIHISI MAUMIVU (Its Ok To Feel Pain) Haiwezi Kuwa Rahisi Kwako Kuachana na Mtu Pasipo Kuumia. Unatakiwa Uumie Ili Ujue "Kweli Huyu Nilimpenda" Na Unatakiwa Kuumia Kama Ishara Kuwa Ndio Anazidi Kukutoka Moyoni. Usiyakwepe Wala Usiyakimbie Maumivu, Yaache Yaje...Ndivyo Anavyokutoka Hivyo. 3. Ni Kawaida KUMMISS Baada Ya Kuachana (Its Ok To Miss Him/Her) Ulipokuwa Nae Kuna Mambo Mliongea, Kuna Mambo Mlifanya. Ambayo Yalitengeneza MEMORIES, Utakapotaka Kuachana Nae Ni KAWAIDA Kuhisi Kama Unammiss. Utamiss Zile Nyakati Mlikuwa Mkicheka. Utamiss Zile Weekends Ambazo Mlikuwa Mnatoka Nje Ya Mji Nk. Unamiss Kumpigia Simu au Kuchat Nae Kwa Sababu Ya Yale Mazoea. Muhimu; Kama Utaachana Nae Mapema Utaumia, Na Hata Ukiachana Nae Hapo Baadae UTAUMIA VILEVILE. Lakini, Maumivu Ya Kuachana Nae Mapema Ni Madogo Kuliko Yale Ya Kusubiri Muda Upite Ndipo Muachane. Mimi Binafsi Nimejifunza Kwamba, Maumivu Ya Kumuacha Mtu Huwa Ni Madogo, Kuliko Maumivu Ya Kuendelea Kuwa Nae Ilihali UMESHAONA WAZI SIO MTU SAHIHI KWAKO. Kubali Kuumia, Maumivu Unayoyasikia Leo Ni Gharama Unalipa Ili Kuinunua Amani Yako. Usisahau...Kuachana Sio Mwisho Wa Upendo, Bali Ni Ishara Ya KUJIPENDA MWENYEWE. By The Way, Kama Umeipenda Makala Hii Fanya Haya: 1. Comment Kitu Ulichojifunza 2. Follow Page Hii Kwa Ajili Ya Mafunzo Zaidi 3. Save Post Hii Kwa Matumizi Ya Baadaye 4. Share Post Hii Ili Iwasaidie Wengine Wengi Isaack Nsumba #Mapenzi #Mahusiano #DarEsSalaam #Tanzania #Uchumba #Ndoa

  • [VIDEO YOUTUBE]; Jinsi Ya Kupenda Tena Baada Ya KUUMIZWA & KUJERUHIKA Mara Kadhaa >>>https://youtu.be/tu0OvX_H0-4?si=Ey2OInAGd8ljk2Ik Ukishatazama Video USISAHAU KUSUBACRIBE